UKRAINE: KATIBU MKUU WA NATO AELEZA MATUMAINI JUU YA KUSITISHA MAPIGANO

UKRAINE: KATIBU MKUU WA NATO AELEZA MATUMAINI JUU YA KUSITISHA MAPIGANO

Like
287
0
Friday, 27 February 2015
Global News

KATIBU MKUU  wa  NATO Jens Stoltenberg  ameonya  kwamba jaribio  lolote  la  kupanua  mipaka  inayoshikiliwa  na  wapiganaji wanaotaka  kujitenga  nchini  Ukraine , halitakubalika  na kuiambia Urusi  kuondoa  vifaa  1,000  vya  kijeshi  kutoka  katika  ardhi  ya nchi  jirani  ya  Ukraine.

Akizungumza  baada  ya  mkutano  na  waziri  mkuu  wa  Italia Matteo Renzi , katibu  mkuu  wa  NATO  ameeleza  matumaini ya tahadhari  juu  ya  matarajio  ya  makubaliano tete  ya  kusitisha mapigano  kati  ya  waasi  wanaoungwa  mkono  na  Urusi  na majeshi  ya  Ukraine.

Matamshi  ya  Stoltenburg  yanakuja  wakati  jeshi  la  Ukraine limetangaza  kuanza  kuondoa  silaha  kali  kutoka  katika  mstari  wa mbele  wa  mapambano.

 

Comments are closed.