UKRAINE: MATAIFA YAOMBA KUFANYIKA MKUTANO WA KILELE

UKRAINE: MATAIFA YAOMBA KUFANYIKA MKUTANO WA KILELE

Like
259
0
Monday, 09 February 2015
Global News

VIONGOZI wa Ukraine, Ujerumani na Ufaransa wanashinikiza kuwepo kwa mkutano wa kilele na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumatano wiki hii katika juhudi za hivi karibuni  za kuutafutia ufumbuzi mzozo wa mashariki mwa Ukraine.

Hata hivyo Rais Putin ameonya kuwa mkutano huo unaotarajiwa kufanyika mjini Minsk, utafanyika tu iwapo viongozi hao watasikilizana kuhusu masuala kadhaa kabla ya Jumatano.

Hii leo maafisa wa wizara ya mambo ya nje wa nchi hizo nne watafanya mazungumzo kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo wa kilele mjini Berlin.

Comments are closed.