UKRAINE: PANDE MBILI ZINAZOPIGANA ZAJUTIA KUTOSITISHA MAPIGANO

UKRAINE: PANDE MBILI ZINAZOPIGANA ZAJUTIA KUTOSITISHA MAPIGANO

Like
219
0
Thursday, 19 February 2015
Global News

OFISI ya Rais nchini Ufaransa imesema Viongozi wa Urusi,Ukraine, Ufaransa na Ujerumani wamekemea ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine .

Baada ya Mazungumzo ya simu kati ya Viongozi wanne wa Nchi hizo,wametoa wito wa utekelezwaji wa makubaliano yaliyowekwa mjini Minsk Juma lililopita, ikiwemo kuacha kabisa mapigano.

Waangalizi wa Kimataifa wanaofuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo nchini Ukraine wamesema pande zote mbili zinajutia kushindwa kutekeleza makubaliano hayo.

Comments are closed.