Kampuni ya azimio estate iliyompa zawadi mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda inadaiwa kuhusika na wizi mkubwa wa pesa ya umma, baada ya kampuni hiyo kuingia mkataba na Shirika la taifa la hifadhi ya jamii (Nssf) wakuiuzia ardhi ekari 20,000 eneo la Dege Mbutu Kigamboni kwa makubaliano ya kila eka moja ni miloni ishirini na tano ( 25,000,000/=), serikali ikalipa pesa yote.
Serikali imekuja kupewa eka 3,000 tu hali inayotafsiriwa kuwa sasa imeuziwa eka moja kwa zaidi milioni mia nane (800,000,000/=).
Bunge kupitia kamati yake imeiagiza takukuru kuchunguza wizi huu, ambapo kampuni hiyo imekiri udanganyifu huo na ikaamriwa
kurudisha pesa na kusaini mkataba upya wa eka 3,000 zilizopo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Nssf, Prof Godius Kahyarara amekiri kuingia ubia na kampuni ya azimio lakini taarifa sahihi ni kwamba hawakuuziana kama inavyoelezwa
bali wameingia ubia na mfanyabiashara huyo mohammed iqbal.