ULAYA YAKUBALI KUIPA UGIRIKI MKOPO MWINGINE

ULAYA YAKUBALI KUIPA UGIRIKI MKOPO MWINGINE

Like
245
0
Monday, 13 July 2015
Global News

VIONGOZI wa mataifa ya ulaya yanayotumia sarafu ya Euro wamekubaliana kwa pamoja kuipa Ugiriki mkopo mwingine ili kuinusuru uchumi wake kuporomoka zaidi.

Makubaliano hayo yamejiri baada ya mazungumzo ya dharura baina ya mawaziri wa fedha wa ukanda wa Ulaya waliodhamiria kuiokoa nchi hiyo kiuchumi kutokana na kupungukiwa fedha.

Rais wa baraza la ulaya Donald Tusk ametangaza kuwa makubaliano yameafikiwa baada ya mazungumzo hayo marefu yaliyochukua takriban saa kumi na saba ambapo amesema pia kabla ya kutumika makubaliano hayo yatahitajika kuidhinishwa na mabunge kadhaa ikiwemo bunge la Ugiriki.

Comments are closed.