UMOJA wa mataifa umeelezea masikitiko yake dhidi ya mataifa kadhaa ya bara la Ulaya, namna yanavyozingatia sheria mbalimbali zinazokinzana kuhusiana na mipaka yake.
Shirika linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa hatua hii itawaacha maelfu ya wakimbizi katika hali ya kutatanika kisheria.
Shirika hilo la UNHCR, limesema kwamba muungano wa bara la Ulaya, unatakiwa kuandaa vituo vya kuwapokea wahamiaji, kuwaandikisha na kuwapiga msasa wahamiaji na wale wanaotafuta makao huko hasa wanaowasili nchini Ugiriki, Italia, na Hungary.