KATIKA kuhakikisha huduma za afya ya uzazi zinawafikia akina mama na vijana waishio pembezoni mwa miji na Vijijini, Chama cha Uzazi na Malezi – UMATI, kimeanza kuendesha huduma mkoba itakayowarahisishia watu wa makundi hayo kufikiwa na huduma kiurahisi katika makazi yao.
Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa -UMATI- Lulu Mwanakilala amesema katika huduma Mkoba Wataalamu wa afya watawafata akina mama na Vijana katika makazi yao wakiwa na vifaa vyote vya kutolea huduma za afya ya uzazi kwa lengo la kuwapunguzia safari ndefu kuelekea katika vituo vya afya.