JUMUIYA ya Kimataifa imekumbushwa kuisaidia Tanzania katika kuhudumia wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Kongo ambao wanaishi kwenye kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Kigoma.
Rodriguez amesema kwamba serikali ya Tanzania kwa miaka mingi imekuwa ikikubali kusaidia majirani zake kwa kuhifadhi wakimbizi na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kuona hilo na kuisaidia Tanzania kufanikisha hifadhi ya wakimbizi