UMOJA WA ULAYA KUISAIDIA HUNGARY JUU YA ONGEZEKO LA WAHAMIAJI

UMOJA WA ULAYA KUISAIDIA HUNGARY JUU YA ONGEZEKO LA WAHAMIAJI

Like
178
0
Wednesday, 26 August 2015
Global News

UMOJA wa Ulaya umesema uko tayari kuisaida Hungary kulishughulikia ongezeko la wahamiaji wanaovuka mipaka yake.

Umoja huo umesema utaipa nchi hiyo kile kinachoitwa kuwa ni hadhi ya ‘eneo hatari la uhamiaji’, ikiwa na maana kuwa nchi hiyo ipewe raslimali za ziada kupambana na hali hiyo.

Hayo yanajiri baada ya serikali ya Hungary kusema kuwa zaidi ya wakimbizi 2,000 waliingia nchini humo hapo jana wiki hii pekee nakuifanya nchi hiyo ikabiliwe na changamoto ya kuwasili nchini humo raia wa nchi jirani zikiwemo Kosovo, Serbia na Bosnia, kufuatia hatua ya hivi karibuni ya kuondolewa vikwazo vya kusafiri.

Comments are closed.