UMOJA WA ULAYA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI

UMOJA WA ULAYA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI

Like
194
0
Tuesday, 29 September 2015
Global News

UMOJA wa Ulaya umesema utaanza kukabiliana na wafanyibiashara wanaowasafirisha wahamiaji kinyume na sheria katika bahari ya Mediterania.

Taarifa kutoka Umoja huo zinaeleza kuwa upo uwezekano wa kuanzisha operesheni ambayo itaruhusu majeshi ya nchi wanachama kuingia, kufanya upekuzi na kuzuia boti ambazo zinashukiwa kuhusika katika biashara haramu ya kuwasafirisha wahamiaji kuanzia oktoba saba mwaka huu.

Hata hivyo viongozi wa dunia waliopo katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wamezihimiza nchi za Umoja wa Ulaya kuwakaribisha wahamiaji na kuzisaidia kifedha nchi za mashariki ya kati zinazowafadhili wakimbizi.

Comments are closed.