VIONGOZI wa Taifa na Serikali wa nchi za Umoja wa Ulaya wamekubaliana kurefusha vikwazo vya Kiuchumi dhidi ya Urusi hadi Desemba mwaka huu.
Katika mkutano wao wa kilele mjini Brussels viongozi hao wa Mataifa 28 wamefungamanisha vikwazo hivyo na kuheshimu makubaliano ya kuweka chini silaha na kurejesha amani Mashariki mwa Ukraine.
Hata hivyo Viongozi hao wamezidi kumshinikiza Rais wa Urus VLADIMIR PUTIN, atumie ushawishi wake kuwatanabahisha Waasi wanaoelemea upande wa Urusi ili kumaliza mzozo wa Mashariki mwa Ukraine.