UMOJA WA ULAYA WAFIKIA MAKUBALIANO JUU YA WAKIMBIZI KUTOKA SYRIA

UMOJA WA ULAYA WAFIKIA MAKUBALIANO JUU YA WAKIMBIZI KUTOKA SYRIA

Like
294
0
Wednesday, 04 May 2016
Global News

UMOJA wa Ulaya na Uturuki wamekubaliana, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya Habari juu ya namna ya kuwachagua wakimbizi wa Syria watakaohamishiwa katika nchi za Umoja huo.

Gazeti la “Bild” limenukuu waraka wa siri unaoonyesha kwamba wasyria tu ndio watakaoruhusiwa kwanza kuingia katika nchi za Umoja wa ulaya ikiwa wameomba kinga kabla ya novemba 29 nchini Uturuki.

Aidha taarifa zimeeleza kwamba Makubaliano ya awali yanawataka wakimbizi kutojichagulia wenyewe nchi wanayotaka wapelekwe na badala yake kukubali kupangiwa nchi za kwenda.

Comments are closed.