UMOJA WA ULAYA WALAANI HATUA YA RAIS WA MACEDONIA KUWASAMEHE WANASIASA WALIOHUSISHWA NA UFISADI

UMOJA WA ULAYA WALAANI HATUA YA RAIS WA MACEDONIA KUWASAMEHE WANASIASA WALIOHUSISHWA NA UFISADI

Like
225
0
Wednesday, 13 April 2016
Global News

MUUNGANO wa ulaya umelaani hatua ya rais wa Macedonia, Gjorge Ivanov, kuwasamehe wanasiasa waliohusishwa na ufisadi.

Kamishna anayehusika na upanuzi wa muungano huo Johannes Hahn, amesema kuwa msamaha huo hauambatani na uelewa wake wa sheria na hivyo, unahatarisha lengo la Macedonia kuwa mwanachama wa muungano huo.

Taifa hilo limekumbwa na mzozo unaohusiana na madai kwamba chama tawala na wakuu wa idara ya ujasusi , walidukua simu za zaidi ya watu alfu ishirini wakiwemo waandishi wa habari na maafisa wa idara ya mahakama.

Comments are closed.