UMOJA WA ULAYA WAONYESHA MATUMAINI HISPANIA

UMOJA WA ULAYA WAONYESHA MATUMAINI HISPANIA

Like
236
0
Tuesday, 22 December 2015
Global News

RAIS wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker, amesema kuwa umoja huo una matumaini kwamba hispania itaunda serikali imara, kufuatia uchaguzi ambao waziri mkuu Mhafidhina Mariano Rajoy, amepoteza viti vingi vya Ubunge kwa vyama vya mrengo wa kushoto.

Juncker amewambia wandishi wa habari mjini Brussles kuwa amezingatia matokeo ya uchaguzi huo na maelezo ya hisia za Wahispania na kuongeza kuwa zipo juu ya mamlaka ya nchi hiyo katika kuunda serikali inayoweza kutimiza wajibu wake.

Hata hivyo vyama vya mrengo wa kushoto vimetangaza kuwa havitashiriki katika serikali atakayoiunda Waziri huyo huku baadhi vikitangaza adhima ya kumzuia kuiunda serikali hiyo ya muungano.

Comments are closed.