UN: KOREA KASKAZINI INASTAHILI KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU

UN: KOREA KASKAZINI INASTAHILI KUFIKISHWA KWENYE MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA UHALIFU

Like
270
0
Wednesday, 19 November 2014
Global News

BARAZA la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu limesema Korea Kaskazini inastahili kufikishwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu kutokana na kukiuka haki za binadamu.

Katika baraza hilo zimetolewa tuhuma dhidi ya Korea Kaskazini kwamba serikali yake imekuwa ikifanya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu.

Mapendekezo hayo yaliyopitishwa na baraza la haki za binadamu la kimataifa yanapaswa kupigiwa kura ili kupitishwa na bunge yaweze kuhalalishwa.

Ripoti ya mwezi Februari mwaka huu iliyotolewa na umoja wa mataifa ilibainisha kuwa watu wa Kawaida Korea Kaskazini wanakabiliwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na pia mauaji.

Comments are closed.