MKUTANO mKuu wa Umoja wa Mataifa umeunga mkono kwa kauli moja azimio linalotoa wito kwa Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya Cuba.
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilipata kura 191 dhidi ya 2 kulaani vikwazo vya kibiashara, kiuchumi na kifedha ambavyo Marekani imeliwekea taifa hilo la kikomunisti.
Hata hivyo ingawa kura hizo zilipigwa bado Marekani ilipiga kura ya kupinga azimio hilo la Vikwazo vilivyowekwa tangu mwaka 1960, wakati wa kilele cha Vita Baridi, Marekani ilipovunja mahusiano yake na Cuba.