UNAFAHAMU KIASI CHA PESA WALICHOLIPWA SAUTI SOL KWENYE SHOW MBELE YA OBAMA?

UNAFAHAMU KIASI CHA PESA WALICHOLIPWA SAUTI SOL KWENYE SHOW MBELE YA OBAMA?

Like
332
0
Thursday, 30 July 2015
Entertanment

Bendi ya muziki wa afro pop kutokea Kenya hivi karibuni imeingia kwenye Headlines za vyombo vikubwa vya habari ulimwenguni baada ya kutumbuiza katika hafla ya chakula cha usiku katika ikulu ya nchi iliyoandaliwa na rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta akimakrimu rais wa marekani Barack Obama alipotembelea taifa hilo lililobeba histaoria ya maisha ya kiongozi huyu.

 

Katika show hiyo ya Sauti Sol aliyofanyika ikulu Rais Obama pia aliungana na vijana hao kucheza muziki mzuri kutoka kwenye bendi hiyo.

 

Wengi huenda wakawa wanajiuliza muda huu ni kiasi gani cha fedha bendi hiyo ililipwa kutumbuiza katika tukio hilo la kihistoria lakini jibu ni hakuna malipo waliyopokea kutokana na show hiyo hii ni kwa mujibu wa tovuti ya Ghafla ya nchini Kenya.

 

Huenda pesa isiwe na thamani sawa na faida waliyoipata wasanii wa bendi hii kufuatia nafasi waliyoipata na faida mbalimbali wanazotarajia kuzipata kutokana na kuonekana na dunia nzima na kuwafanya wajulikane kama bendi inayotambulika kimataifa.

Hongera na pongezi kwa sauti Sol bendi itakayovuna matunda ya uzalendo kwa taifa la Kenya

https://youtu.be/oW519QJOwRk

Comments are closed.