UNESCO YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

UNESCO YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

Like
343
0
Monday, 27 July 2015
Local News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni –UNESCO- limeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa uvumbuzi kupitia elimu bora.

 

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

 

Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT unaoendeshwa na shirika hilo na serikali ya China kwa lengo la kuisaidia Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kupitia Tehama.

UN2

Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.

 

 

 

UN3

Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu”UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania” wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.

Comments are closed.