UNESCO YAENDESHA WARSHA KWA WAKUU WA HIFADHI NA VITUO VYA UTALII

UNESCO YAENDESHA WARSHA KWA WAKUU WA HIFADHI NA VITUO VYA UTALII

Like
299
0
Monday, 12 October 2015
Local News

Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Idara ya mambo ya kale imeendesha warsha ya siku moja kwa wakuu wa hifadhi na vivutio vya utalii nchini kwa lengo la kushirikishana masuala muhimu yanayohusu utalii.

 

Warsha hiyo iliyohudhuriwa na Wakuu wa hifadhi mbalimbali nchini imehusisha uwasilishaji wa mafanikio na changamoto wanazokutana nazo wakuu wa hifadhi hizo huku matatizo makubwa yakiwa ni Ukosefu wa fedha kwaajili ya Kujiendesha.

 

Akizungumza katika warsha hiyo Mkuu wa Hifadhi ya Usambara Mashiriki Mwanaidi Kijazi amesema kuwa Mbali na Changamoto nyingi zinazojitokeza katika hifadhi za jamii lakini bado kuna mafanikio mengi yaliyojitokeza ikiwemo kutoa nafasi za Ajira kwa watanzania wengi na kukuza pato la Taifa.

DSC_3586

Baadhi ya washiriki wa warsha iliyoandaliwa na UNESCO pamoja na Idara ya Mambo ya Kale wakiwa katika picha ya pamoja

Comments are closed.