UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI NA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

UNESCO YAKUTANISHA WADAU KUJADILI NA KUHAMASISHA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Like
300
0
Tuesday, 06 October 2015
Local News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) limewakutanisha wadau mbalimbali katika kongamano la kujadili na kuhamasisha Amani katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kongamano hilo lililofanyika wilayani Simanjiro mkoani Manyara limewakutanisha viongozi wa dini, mila na wawakili wa muungano wa Redio za Jamii nchini ambao kwa pamoja walisisitiza umuhimu wa Amani.

Ofisa Miradi wa Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph amesema kuwa mchango unaotolewa na Redio za kijamii nchini ni mkubwa kwani unawawezesha wananchi kuzitumia kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali.

UN-3

Mjumbe wa Bodi ya Muungano wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Balozi Christopher Liundi akichangia mada ya umuhimu wa matumizi ya Redio za Jamii.

Comments are closed.