UNHCR KUTOA URAIA KWA WATU MILIONI 10 ULIMWENGUNI

UNHCR KUTOA URAIA KWA WATU MILIONI 10 ULIMWENGUNI

Like
238
0
Tuesday, 04 November 2014
Global News

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi – UNHCR limeanzisha kampeni inayolenga kumaliza tatizo la watu wasio na uraia wa nchi yoyote, ambao kwa mujibu wa shirika hilo wanafikia milioni 10 kote ulimwenguni.

Mkurugenzi wa Shirika hilo ANTONIO GUTERRES amesema hali ya watu hao haikubaliki hata kidogo, na kuongeza kuwa lengo ni kuwa tatizo lao liwe limepatiwa ufumbuzi wa kudumu katika muda wa miaka 10.

UNHCR imesema kupitia kampeni hiyo inataka kuziangazia changamoto wanazokabiliana nazo watu wasio na uraia na kuzihimiza nchi kuzirekebisha sheria zao ili pasiweko na mtu anayejikuta katika hali ya kutokuwa raia wa nchi yoyote.

Comments are closed.