UPINZANI KUTAMBULISHA USIMAMIZI WA KODI GES NA MAFUTA

UPINZANI KUTAMBULISHA USIMAMIZI WA KODI GES NA MAFUTA

Like
276
0
Thursday, 13 November 2014
Local News

KAMBI rasmi ya upinzani Bungeni imeitaka Serikali kuhakikisha kuwa inaandaa na kutambulisha Mfumo Rasmi na Imara wa Usimamizi wa Kodi katika sekta ya Gesi na Mafuta ili kuleta tija na maslahi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Msemaji wa Kambi hiyo Mheshimiwa JAMES MBATIA wakati akitoa mapendekezo ya kambi hiyo mara baada ya Waziri wa Fedha Mheshimiwa SAADA MKUYA kusoma kwa mara ya pili Muswada wa Usimamizi wa Kodi wa mwaka 2014.

Baadhi ya mapendekezo kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani kwa serikali ni kuwezesha na Kuunda Chombo muhimu cha usimamizi wa Kodi kwa Wananchi pamoja na kuanzisha na kuweka Masharti ya Usimamizi.

Comments are closed.