Mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu wa Cameroon Maurice Kamto anadai kuwa ameshinda uchaguzi wa uraisi wa siku ya jumapili licha ya onyo la serikali dhidi ya hatua.
Kamto ambaye ni kiongozi wa chama cha Rebirth of Cameroon (MRC), ametoa wito kwa rais Paul Biya kuachia madaraka kwa amani.
Akizungumza na waandishi wa habari mji mkuu wa Yaounde amesema ”Namuomba rais anayeondoka kupanga namna ya kumpokeza madaraka mpizani wake kwa amani”