UPOTEVU WA VYETI NA NYARAKA NI CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKRETARIETI YA AJIRA NA UTUMISHI WA UMMA

UPOTEVU WA VYETI NA NYARAKA NI CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKRETARIETI YA AJIRA NA UTUMISHI WA UMMA

Like
435
0
Wednesday, 23 December 2015
Local News

SEKRETARIETI ya Ajira katika Utumishi wa Umma katika kutekeleza jukumu lake la uendeshaji wa mchakato wa ajira serikalini, imekuwa ikikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ya matukio ya upotevu wa vyeti vya kitaaluma na nyaraka nyingine za msingi kutoka kwa waombaji kazi.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imeeleza kuwa waombaji kazi laki 256,928 wamekosa nafasi ya kuitwa kwenye usaili ili kuweza kuajiriwa Serikalini kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kutokuwa na vyeti vya kitaaluma, kutozingatia vigezo vya tangazo la kazi, pamoja na kuomba nafasi ya kazi ambayo mwombaji hana sifa zinazokidhi nafasi hiyo.

Comments are closed.