NCHI ya Urusi imesema kuwa inatafakari uwezekano wake wa kuifuata Marekani ili kuwashambulia kwa ndege wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS).
Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ameyasema hayo baada ya kukutana na Rais wa Marekani Barack Obama kwenye maongezi ya nje ya mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN).
Hata hivyo hotuba zilizotolewa na viongozi hao katika mkutano huo, ziliashiria mgawanyiko kuhusu jinsi ya kumaliza vita nchini Syria ambapo Urusi ilisema itakua “kosa kubwa” kutofanya kazi na Rais wa Syria Bashar al-Assad kukabiliana na IS.