URUSI na Marekani zimetia saini makubaliano yanayotarajiwa kuzuia ndege za kijeshi za nchi hizo kushambuliana nchini Syria.
Habari za kutiwa saini kwa mkataba huo zimethibitishwa na maafisa kutoka nchi zote mbili.
Urusi ilianza kushambulia kwa ndege maeneo ya Syria Septemba 30, ikisema ilikuwa ikiwalenga wapiganaji wa kundi la Islamic State –IS, Nna wiki iliyopita, Marekani ilisema ndege za mataifa hayo zilikuwa zimeingia eneo moja la mapigano na zilikuwa karibu sana kukutana.