MELI nne za kijeshi za Urusi zimeshambulia maeneo ya kundi la Dola la Kiislamu nchini Syria kwa makombora, hii ikiwa ni moja kati ya kampeni zake za kijeshi kulishambulia kundi hilo.
Rais Vladimir Putin ameelezwa na waziri wake wa ulinzi Sergei Shoigu kwamba pamoja na ndege za kijeshi, meli nne za kijeshi kutoka eneo la bahari ya Caspian zimeshiriki katika hujuma hiyo na kuongeza kwamba meli hizo za kijeshi zimefanya mashambulizi 26 ya makombora dhidi ya maeneo 11 ya kundi la IS.
Wakati huo huo waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema leo kwamba Marekani haitashirikiana na Urusi kijeshi nchini Syria kwa kile alichosema mkakati wa nchi hiyo una mapungufu mengi.