URUSI YAONYA KULIPA KISASI KUFUATIA KUANGUSHWA KWA NDEGE YAKE

URUSI YAONYA KULIPA KISASI KUFUATIA KUANGUSHWA KWA NDEGE YAKE

Like
243
0
Wednesday, 25 November 2015
Global News

URUSI imeonya kuwa italipiza kisasi kufuatia kuangushwa kwa ndege yake.

 

Waziri mkuu wa Urusi , Dmitriy Medvedev, amesema kuwa Uturuki inawalinda Islamic State na kufafanua kuwa nchi hiyo inahofia kupoteza kipato kikubwa inachofaidika kutokana na wizi wa mafuta kutoka Syria.

 

Hayo yamejiri huku rais wa Marekani Barack Obama amemhakakishia mwenzake rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kuwa nchi yake inaiunga mkono Uturuki katika jitihada za kulinda mipaka yake.

Comments are closed.