US OPEN: ANDY MURRAY ATOLEWA

US OPEN: ANDY MURRAY ATOLEWA

Like
195
0
Tuesday, 08 September 2015
Slider

Mcheza Tenisi Andy Murray ameyaaga mashindano ya US Open baada ya kuchapwa na Kevin Anderson wa Afrika ya kusini.

Mwingereza huyo ameondolewa katika michezo hiyo baada ya kubugizwa seti 7-6 (7-5) 6-3 6-7 (2-7) 7-6 (7-0).

Katika upande wa wanawake mwingereza mwingine Johanna Konta akapokea kichapo cha 7-5 6-3 kutoka kwa Petra Kvitova wa Czech.

Sasa Kelvin Anderson anatakutana na Wawrinka ambaye amempiga mmarekani Donald Young.

Ukiacha mchuano huo, nadhani pambano linalosubiriwa na wengi sasa ni linalowakutanisha mabinti wa Mzee Williams, Serena na Dada yake Venus.

Comments are closed.