UTAFITI: WATOTO WASIOWEZA KUUGUA UKIMWI

UTAFITI: WATOTO WASIOWEZA KUUGUA UKIMWI

Like
244
0
Thursday, 29 September 2016
Slider

Uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa chuo cha Oxford umeonysha kuwa asilimia 10 ya watoto walioambukizwa virusi vya HIV hawapati ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutopata matibabu.

Utafiti uliofanyiwa watoto 170 walio na virusi vya HIV nchini Sudan Kusini ulionyesha kuwa kinga yao ya mwili ililingana na ya nyani waliokuwa na virusi hivyo.

Wataalamu wanasema kuwa ugunduzi huo ni ishara ya kwanza ya watu wanoishi na virusi vya HIV, ambao utasababisha kupatikana na tiba kwa wagonjwa wote walio na virusi hivyo.

Ikiwa virusi vya HIV haviwezi kutibiwa vinaweza kuwaua asilimia 60 ya watoto walio na virusi hivyo katika kipindi cha miaka miwili unusu.

Kisha virusi hivyo huua kinga yote ya mwili na kuacha mwiwi kwenye hatari ya kuambukizwa maradhi mengine.

Watafiti walichunguza damu kutoka kwa watoto 170 kutoka Sudan Kusini waliokuwa na virusi vya HIV, ambao hawakupata matibabu na ambao hado hawakuwa wameugua ugonjwa wa ukimwi.

Comments are closed.