UTATA JUU YA KIFO CHA OSAMA BIN LADEN

UTATA JUU YA KIFO CHA OSAMA BIN LADEN

Like
886
0
Friday, 07 November 2014
Global News

UTATA  umetanda miongoni mwa wananchi nchini Marekani kutaka kujua ni askari yupi hasa aliyefyatua risasi iliyomuua Osama Bin Laden, zaidi ya miaka mitatu baada ya kifo cha kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, baada ya kuibuka madai mbalimbali.

Askari wa zamani wa kikosi cha Seal cha wanamaji wa Marekani, Robert O’Neill, mwenye umri wa miaka 38, ameliambia gazeti la Washington Post katika mahojiano mapya kuwa ndiye alifyatua risasi iliyomuua Osama.

Maelezo hayo yanapingana na yale ya Matt Bissonnette, askari mwingine wa zamani wa kikosi cha Seal aliyeshiriki katika operesheni ya kumsaka kwenye maelezo yaliyotolewa katika kitabu mwaka 2012.

 

Comments are closed.