UTAWALA wa serikali ya kidini katika mji mkuu wa Tripol nchini Libya umekabidhi mamlaka kwa viongozi wanaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Uamuzi huo ulichapishwa katika mtandao wa wizara ya sheria.
Mamlaka mpya ya Libya wiki iliyopita imehamia mji mkuu,Tripoli katika harakati za kutaka kutawala nchi nzima, huku kukiwa na ngome nyingine mbili tofauti za utawala Mashariki mwa nchi hiyo.
Hatua hii ni matokeo ya jitihada za umoja wa mataifa kuunda serikali ya pamoja ili kuweza kuondoa mgawanyiko wa utawala ndani ya taifa hilo ulioanza kushamiri tangu wakati wa machafuko mara tu baada ya kuangushwa kwa utawala uliokuwepo.