CHAMA cha AK cha Uturuki kimepata viti vingi vya bunge vitakavyoweza kudhibiti bunge la nchi hiyo baada ya kupoteza miezi mitano iliyopita.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutangazwa kwa siku kadhaa zijazo lakini karibu kura zote zimeshahesabiwa ambapo chama hicho cha AK kimejikusanyia zaidi ya asimilia hamsini kutawala bunge.
Matokeo hayo yatampa nguvu rais Recep Tayyip Erdogan ambaye aliita kura hiyo kama kura ya amani na ujumbe kwa wanamgambo wa kikurdi na kudai kuwa vurugu haziwezi kuishinda demokrasia.