SERIKALI ya Uturuki imesema itawaalika wawekezaji kutoka
nchini humo ili waweze kutumia nafasi za uwekezaji zilizopo katika Hifadhi za Taifa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na balozi wa Uturuki nchini, Yasemine Eralp alipotembelea Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha na kukutana na viongozi wa shirika.
Balozi Eralp amesema kuwa sekta ya utalii ni miongoni mwa vipaumbele vyake na kwamba atatumia muda wake mwingi kuhakikisha kuwa sekta hiyo inastawi na kuvutia watalii wengi nchini kutoka Uturuki huku akitoa nafasi kwa TANAPA kujitangaza katika Jarida la Shirika la Ndege la Uturuki la Skyline Magazine.
UTURUKI KUWAALIKA WAWEKEZAJI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI