UTURUKI YAAPA KUTOLEGEZA KAMBA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA WANAMGAMBO WA KIKURDI

UTURUKI YAAPA KUTOLEGEZA KAMBA KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA WANAMGAMBO WA KIKURDI

Like
189
0
Wednesday, 12 August 2015
Global News

RAIS wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameapa kutolegeza kamba katika operesheni ya kijeshi inayoendelea dhidi ya wanamgambo wa Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi, PKK.

Erdogan ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye sherehe ya kijeshi, wakati serikali yake ikianzisha mashambulizi mapya dhidi ya waasi wa kikurdi ndani ya mipaka ya Uturuki.

Wiki hii ndege za jeshi la Uturuki zimefanya mashambulizi kuvilenga vituo 17 vya wakurdi katika mkoa wa Hakkari, katika juhudi mpya dhidi ya chama cha PKK ambacho kimepigwa marufuku.

Comments are closed.