UTURUKI YAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA WAKURDI SYRIA

UTURUKI YAENDELEZA MASHAMBULIZI DHIDI YA WAKURDI SYRIA

Like
231
0
Monday, 15 February 2016
Global News

UTURUKI imeendelea kuyashambulia maeneo ya Wakurdi nchini Syria kwa siku ya pili, licha ya kuongezeka shinikizo la kimataifa kuitaka nchi hiyo isitishe mashambulizi yake kwenye eneo la mpakani.

Uturuki inataka wapiganaji wa Kikurdi waondoke kwenye eneo hilo la mpaka.

Akizungumza kwa njia ya simu na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Uturuki, Ahmet Davutoglu amesema vikosi vya usalama vya nchi yake havitowaruhusu Wakurdi wafanye vitendo vya uchokozi.

Syria imeyalaani mashambulizi ya Uturuki, huku ikiutolea wito Umoja wa Mataifa kuchukua hatua.

 

Comments are closed.