VAN DER GOUW: VALDES NI MBADALA WA DE GEA

VAN DER GOUW: VALDES NI MBADALA WA DE GEA

Like
268
0
Tuesday, 19 May 2015
Slider

Manchester United tayari ian mtu sahihi wa kusimama mbadala wa David De Gea, hivyo kipa huyo machachari wa Hispania anaweza kwenda kuitumikia Real Madrid hii ni kwa mujibu wa kipa wa zamani wa Manchester Raimond van der Gouw.

Man U ilimsajiri Victor Valdes, 33, mapema January na Van der Gouw anaamini kipa huyu anakila sababu ya kuwa kileleni

De Gea, 24, amemaliza mkataba wake na Man U katika msimu ujao wa kiangazi richa ya kutosaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Meneja wa Man U Louis van Gaal anaamini kuwa ofa itakayoletwa na Real Madrid itampa wakati mgumu kipa huyo kufanya maamuzi.

De Gea alijiunga na klabu hiyo mwaka 2011 akitokea Atletico Madrid na amekuwa mchezaji bora wa klabu wa mwaka katika msimu uliopita.

Kwa mujibu wa Van der Gouw aliewahi kuichezea Man U kati ya mwaka 1996 hadi 2002, amesema Valdes anauzoefu wa kukabiliana na mchakamchaka wa klabu kama Man U

Comments are closed.