VAN PERSIE KUENDELEA KUKIPIGA MANCHESTER UNITED

VAN PERSIE KUENDELEA KUKIPIGA MANCHESTER UNITED

Like
240
0
Tuesday, 07 July 2015
Slider

Agenti wa mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie amepuuzilia mbali uvumi mteja wake amekubali kuondoka Manchester United na kujiunga na majabali wa Uturuki, Fenerbahce.

Taarifa zilitapakaa wikendi iliyopita kuwa straika huyo amewekwa sokoni na miamba hao wa ligi Premier Uingereza na amekubali kufunga virago vyake kuhamia klabu hicho cha Super Lig baada ya kukubaliana matakwa binafsi.

Kess Vos alikanusha ripoti hizo akisema mshambuliaji huyo nyota, 31, ataendelea kufanya matayarisho wa msimu ujao Old Trafford kama ilivyotarajiwa.

“Ikiwa Robin amepata klabu kipya, tungetoa tangazo rasmi. Niko Uholanzi kwa sasa na kile naweza kusema pekee ni kuwa atajiunga na wenzake wa Manchester United kwa mazoezi,” Voss aliambia Voetbal International.

Van Persie alifika Old Trafford Jumatatu kuanza matayarisho ya kampeni ijayo.

Comments are closed.