VICTOR VALDES KUUZWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

VICTOR VALDES KUUZWA KWA UTOVU WA NIDHAMU

Like
237
0
Thursday, 16 July 2015
Slider

Meneja wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ametangaza uamuzi wake wa kumuuza mlinda mlango Victor Valdes huku sababu ya msingi ikiwa ni utovu wa nidhamu.

Hatua hiyo inakuja baada ya mlinda mlango huyo kukataa kucheza kwenye kikosi cha pili ndani ya Manchester United.

Van Gaal amesema mlinda mlango huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona ambae alimwaga wino mwezi wa kwanza atakutana utakuwa ni mwisho wake kuitumikia klabu hiyo baada ya kushindwa kufuata filosofia za meneja huyo

“kama hutaki kufuata sheria na misingi basi njia ni moja tu nayo ni kuondoka” alisema Van Gaal wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alifunguka juu ya usajili na safari yao ya Marekani mwanzoni mwa msimu

Comments are closed.