VIDEO: TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI: MTU MMOJA AKUTWA AMEKUFA KIMARA TEMBONI

VIDEO: TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI: MTU MMOJA AKUTWA AMEKUFA KIMARA TEMBONI

Like
947
0
Monday, 26 January 2015
Local News

MTU MMOJA asiyejulikana amekutwa amekufa katika eneo la Kimara Temboni, Mtaa wa Upendo.

EFM imefika katika eneo hilo na kushudia mwili wa mtu huyo ukiwa umeharibika vibaya baada ya kukaa muda mrefu bila kugundulika na hivyo kusababisha harufu kali katika eneo hilo.

 

Inasemekana kabla ya mwili huo kuharibika zaidi katika hatua ya kutoa harufu haukuweza kugundulika kwa sababu ulikuwa katika eneo ambalo limejificha na baadhi ya watu kudhani kuwa huwenda ni mnyama amekufa kwakuwa mara nyingi wakazi wa eneo hilo hulitumia kwa kutupa uchafu.

 

Mwili huo umegunduliwa na mtu mmoja aliyepita katika eneo hilo akiwa kwenye shughuli zake za ukataji wa nyasi.

 

Polisi pamoja na Daktari kutoka Hospitali ya Mwananyamala wamefika katika eneo hilo, na kwakushirikiana na Serikali ya mtaa na wananchi waliupekua mwili huo na kukuta marehemu alikuwa na simu ya mkononi katika mfuko wa kulia wa suruali yake ikiwa na line ya mtandao wa Vodacom ambavyo vimechukuliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

 

EFM imezungumza na GEORGE KASHURA Mjumbe wa  Serikali ya Mtaa wa Upendo Kimara Temboni.

 

 

Comments are closed.