Wazazi huko india wameparamia ukuta kupitisha majibu ya mitihani kwa watoto wao
Watoto katika shule ya Bihar wilaya ya Hajipur wamekuwa wakipata msaada wa kupitishiwa majibu na wazazi wanapokuwa kwenye vyumba vya mitihani.
Kwenye mkanda wa video uliorekodiwa na chanzo kimoja cha habari za ndani nchini humo kinaonyesha umati wa wazazi wakiparamia kuta za ghorofa kuwapitishia wanafunzi majibu ya mtihani kwa kutumia madirisha ya jengo hilo
Zaidi ya wanafunzi milioni 1.4 wapo katika mitihani ambayo inarajiwa kumalizika march 24 nchini India lakini udanganyifu katika kanda ya wilaya hiyo imekuwa kitu cha kawaida kabisa richa kuwepo kwa ulinzi wa askari.
Kwa mujibu wa chanzo hicho wanafunzi wamekuwa wakiingia na madaftari pamoja na vitabu ili kujibu mitihani yao.