VIJANA WA MKOANI Kilimanjaro wameziomba Halmashauri zao kuhamasisha vijana kuanzisha SACCOSS za Wilaya zitakazowawezesha vijana kuwekeza na kuwasaidia kuomba mkopo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana utakaopitishiwa katika SACCOSS hizo ili waweze kujiajiri.
Hayo yamesemwa na Vijana wakati wa kufunga Semina ya Uhamasishaji kwa vijana kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kuiomba Wizara yenye dhamana na vijana kujitolea kutoa Elimu kwa vijana mara kwa mara itakayowawezesha vijana kujitambaua na kuwajengea uwezo.