VIJANA nchini wametakiwa kutojihusisha na makundi hatari bila kuwa na kazi yoyote na badala yake wahakikishe wanajikita zaidi katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali ili waondokane na umasikini.
Kauli hiyo imetolewa na Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi-CCM-Silvestry Koka alipokuwa akizungumza na vijana wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa tawi jipya la CCM jimboni hapo.
Koka amesema kuwa baadhi ya vijana wanalalamika kutokuwa na ajira tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa husababishwa na wao kwa kutotaka kujishughulisha.