MAMIA ya vijana wamejitokeza nchini Cameroon kujitolea kuwapa damu wanajeshi wanaopambana na kundi la wapiganaji la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo.
Kampeni hiyo imeandaliwa na baraza la muungano wa vijana nchini humo ambao wamesema kuwa huo ndio mchango wao mkubwa na muhimu dhidi ya ugaidi.
Hospilitali ya kijeshi ya Yaounde ambayo wanajeshi waliojeruhiwa kutoka Cameroon na Chad hupewa matibabu, imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa akiba ya damu ya kutosha.