VIJANA WATAKIWA KUJIAJIRI

VIJANA WATAKIWA KUJIAJIRI

Like
899
0
Wednesday, 08 April 2015
Local News

VIJANA nchini wametakiwa kuacha kubweteka na kusubiri kuajiriwa na badala yake wajiajili wenyewe kwa ujasiliamali pamoja na kilimo cha kisasa.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara wa kutembelea shamba lenye ukubwa wa Ekari 300 lililopo katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambalo linamilikiwa na Shirikisho la Wasanii Tanzania-  SHIWATA,  Mwenyekiti wa Mtandao huo Casim Taalib amesema kuwa mashamba hayo  ni fursa nzuri kwa vijana kujiajiri.

Taalib amesema vijana wamekuwa na dhana tofauti ya kusubiri kuajiriwa  badala ya kutambua kuwa wanaweza kujiajiri katika masuala mbalimbali na wakajikomboa kiuchumi.

Comments are closed.