VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

Like
294
0
Friday, 16 January 2015
Local News

 NAIBU WAZIRI wa Maliasili na Utalii mheshimiwa MAHAMUOD MGIMWA ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini amewataka vijana kujituma na kutumia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na Serikali.

Akizungumza na EFM Mheshimiwa  MGIMWA amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.

Mheshimiwa MGIMWA amewataka vijana wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi na Sayansi na Teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

Comments are closed.