VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KULETA MAENDELEO

VIJANA WATAKIWA KUWA MSTARI WA MBELE KULETA MAENDELEO

Like
219
0
Wednesday, 12 August 2015
Local News

KATIKA kuadhimisha siku ya Vijana Duniani, Serikali imewataka Vijana nchini kujitokeza, kujitolea pamoja na kubadilisha fikra zao na kuwa na fikra chanya ili kuhakikisha kuwa badala ya kuachwa nyuma katika maendeleo, wanakuwa mstari mbele katika kuleta maendeleo na mabadiliko nchini.

 

Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es salaam leo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema, Serikali kupitia Wizara hiyo itashirikiana na Vijana kwa karibu kuhakikisha kuwa Vijana wanawekewa mazingira mazuri ya kujiendeleza ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia.

Comments are closed.