VIKAO VYA BUNGE VYAANZA RASMI LEO

VIKAO VYA BUNGE VYAANZA RASMI LEO

Like
346
0
Tuesday, 04 November 2014
Local News

 

VIKAO vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimeanza leo mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine bunge litakaa kama kamati ya Mipango kwa mujibu wa masharti ya kanuni ya 94 kifungu cha kwanza na kupokea, kujadili na kutoa maoni na ushauri kuhusu bajeti ya Serikali, vyanzo vya mapato pamoja na mapendekezo ya utekelezaji wake.

Baadhi ya Miswada itakayosomwa ni pamoja na muswada wa Sheria ya kodi ya ongezeko la thamani ya mwaka 2014, muswada wa sheria ya Takwimu ya mwaka 2013, muswada wa sheria ya Marekebisho ya sheria ya Ubia baina na Sekta ya Umma na sekta binafsi wa mwaka 2014.

Bunge pia litapokea taarifa ya Kamati teule iliyoundwa Novemba mosi mwaka 2013 ili kuchunguza na kuchambua sera zinazohusu masuala ya ardhi, kilimo, mifugo, maji na uwekeza ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya ardhi.

 

 

Comments are closed.