VIKOSI VYA UFARANSA VIMEWAUA WAPIGANAJI WANNE WA KIJIHADI MALI

VIKOSI VYA UFARANSA VIMEWAUA WAPIGANAJI WANNE WA KIJIHADI MALI

Like
194
0
Thursday, 21 May 2015
Global News

VIKOSI maalum kutoka Ufaransa vimewaua wapiganaji wanne wa kijihadi, wakiwemo viongozi wawili katika shambulizi lililofanyika eneo la kaskazini mwa Mali.

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi nchini Ufaransa mmoja wa wale waliouwawa ni Amada Ag Hama, anyeshukiwa kuhusika katika utekaji nyara na mauaji ya wanahabari wawili wa Ufaransa mwaka 2013.

Ufaransa iliwatuma wanajeshi wake nchini Mali miaka miwili iliyopita wakati wanamgambo wa kiislamu walipotishia kuuteka mji mkuu, Bamako. Wanajeshi 3,000 wa kikosi cha ufaransa bado wapo katika eneo hilo kukabiliana na ugaidi.

Comments are closed.