VINCENT KOMPANY ATETEA MASHABIKI WA MAN CITY

VINCENT KOMPANY ATETEA MASHABIKI WA MAN CITY

Like
210
0
Monday, 02 November 2015
Slider

Nahodha wa klabu ya Manchester City, Vincent Kompany ametetea kitendo cha mashabiki wa klabu hiyo kuzomea wimbo maalum unaotumika katika ligi ya mabingwa.

Nahodha huyo amesema kuwa ni utani kuona Uefa inachunguza klabu yao baada ya mashabiki wao kuzomea na kupuuzia wimbo huo.

Tukio hilo limetokea kabla ya City kuitandika Sevilla 2-1 wakiwa nyumbani mnamo October 21 ambapo kamati ya usimamizi wa nidhamu katika ligi ya mabingwa imefungua mchakato kuichukulia klabu hiyo hatua za kinidhamu iwapo itabainika kuwa na makosa

 

Nahodha huyu ameeleza kuwa hakuna utukufu katika wimbo huo “tumekuwa tukicheza michezo mbalimbali Ulaya ambapo kumekuwa na matukio ya kibaguzi” alisema Kompany.

 

Aidha mlinzi huyo 29, ambae ni raia wa Belgium ameeleza kuwa  Uefa inaweza kufanya vile iwezavyo juu yao lakini kama watu wanaona ni jambo sahihi kufanya walichokifanya basi wanahaki ya kufanya hivyo kwa kuwa hakuna mahali pengine wanapoweza kuonyesha hisia zao na ameenda mbali zaidi kudai wanawaunga mkono mashabiki wao

Comments are closed.